Mlu habadiliki kiasi hiki kwa siku moja Bila shaka Mari ameonja ya ulimwengu tangu aondoke kijiji chao, kijiji cha akina Zidi Ni mfano wa historia fupi ya Mari na Zidi; historia ambayo inapingana na tapo la ubwege
Kupitia Ame, mwandishi anajaribu kutupatia historia ya viongozi wa bara la Afrika. Wazo lakę ni kuwa, viongozi kwa ujumla - wawe Wakoloni au Waafrika,, hawajalifanyia haki bara la Afrika Mwandishi anawasuta viongozi hao kwa kupenda kusema tu pasi na kuchukua hatua zifaazo kutatua matatizo chungu nzima yanayowakumba raia wa kawaida wa bara hili. Anawakebehi kwa njama zao za kutoa hotuba zenye ufasaha wa maneno bila matendo. Ame anasema:
Wewe, lazima umeshapoteza mzee, ndugu,
Rafiki, mwenzi, mpenzi au muhisani kama mimi nilivyompoteza Zidi... lakini tunacheka na kuchekelea kama vile mazigazi yatawarejesha tunafurahi ..na mbele yetu mazigazi... mazigazi... mazigazi . nini basi kama si ndoto na kujidanganya tu?
Maneno makubwa makubwa, manene manene, lakini hayazuii roho kupotea...
Na kesho ndugu yangu ..ni siku yangu na yako.. kesho tutakufa. (uk. 83)
Ni bayana kuwa maneno havawezi kuzuia kifo Jitihada za kuzuia roho kupotea au kukwepa kifo si ashiki ya kiubwege. Kiubwege kifo hushangiliwa na ndicho hatua ya mwisho ya binadamu ulimwenguni, kikomo cha historia yake duni.
53