kuota ndoto ukaelekea kiza.Ni kama kugeuka nyuma na kuelekea mbele iwapo kote kuna kiza.
Kuishi kuzimu ni sawa na kifo Maisha yanayozungukwa na kiza pandę zote yanachukiza. Afrika ni sharti ifuate mikakati inayofaa iii kutia misingi imara ya maendeleo na maisha bora. Watu wa nchi ya Amezidi wamekuwa wakijidanganya kwa muda mrefu, maisha yao ni ya kindoto, ya kiubwege.
Kifo cha Zidi (uk. 84) ni kifo ambacho mtunzi amekitumia kutoa fundisho kwa jamii. Anaelekea kutuambia kuwa kifo cha kimwili cha watu waliofungwa kwa minyororo ya ukoloni, na ukoloni mamboleo, ni upeo wa juu wa kifo cha polepole cha kiroho na kisaikolojia. Suala hili huashiria maisha ya Waafrika katika vipindi vyote vya utawala; kabla ya ukoloni, kipindi cha ukoloni, na uhuru. Inabainika kuwa, hakuna la maana ambalo bara la Afrika limepata Tunaambiwa:
Mbali kule tunatoka na mbali kule tunakokwenda... Na sasa kiza mbele!
Tumetoka huko au pengine hatujatoka...
Pengine tumesimama pale pale, tokea siku ile, au tumepiga hatua nyuma pasi nakujua, pasi na kutambua ...
Na sasa kiza! Kiza kushoto, kiza kulia . kiza nyuma kiza mbele... tumeshatoka huko au hatujatoka? Nawauliza sa!
(kwa hadhira) Tumefika tunakokwenda'7 (uk. 82).
Ame naye anakufa kutokana na hali na mazingira sawa na yale yaliyosababisha kifo cha Zidi. Vifo vya Ame na Zidi vinalingana na kuendeleza ubwege wao. Kuhusu vifo hivi, Wafula (1999:75) anaeleza kwamba kwa mujibu wa tamthilia ya Amezidi, vifo vya
104