Zidi hubadilisha nafsi zao kalika jamii. Kwa mfano wanakuwa mwalimu na mwanafunzi; Bosi na msaidizi wake; na mkaguzi na mkaguliwa.
Kimaisha, tabia hii huonyesha hali ya tamaa na kutotosheka kwa mwanadamu. Binadamu hana furaha, na mara kwa mara hujaribu kutafuta njia ya kujipatia maisha bora. Juhudi zake hata hivyo, huishia ukingoni kwa vile hana uwezo wa kuleta mabadiliko ya maana maishani mwake Hii ndiyo sababu, Ame na Zidi, ingawa wanajaribu kuwa hivi na vile, hawafaulu kuboresha hali ya maisha yao. Ni kejeli kuwa, hata baada ya kusawiriwa kama Bosi na msaidizi wake, na halafu kuiba pesa nyingi, maisha yao bado ni ya kiubwcge Binadamu hana mwelekeo ulimwenguni. Muhimu kwake ni kuzunguka duara lakę duni bila matumaini ya kuona mbele. Foulquie (1947:56) anafafanua hali hii anaposema:
Binadamu anaendesha maisha yake katika giza totoro la usiku kwenye barabara yenye mabonde. Mwingine anaweza kudai kuwa anaweza kungoja hadi wakati wa mchana, lakini ukweli ni kwamba hawezi, kwa vile mchana huo hautafika.
(Tafsiri yetu)
Hali hii hukatisha tamaa na ni dhihirisho kuwa maisha si kitu cha maana, ni usumbufu
112