Zidi: Labda tulivihamisha mimi na wewe
au tuseme tulivihamisha kwa kuvibadilisha kwa nyama mbovu - aaa, tumboo, Ame; linanikeketa... aaa, naona linaanza tena kuniendesha. (uk 77)
Nyama mbovu inayorejelewa hapa ni lile paja la nyama ya ng ombe lililoangushwa na ( 69-70). Paja hilo lilikuwa na maandishi EC, na ni msaada uliotolewa kuwaokoa raia wa Amezidi kutoka kwa tisho la kifo kutokana na ukosefu wa chakula
Kejeli ni kwamba, badała ya paja hilo kuwaokoa wapokeaji, linawaletea ugonjwa mbaya kusababisha kifo chao. Kifo cha Ame na Zidi kinathibitisha imani ya kidhanaishi kuwa, binadamu hana uwezo wa kuzuia kifo, kifo ndicho hatua ya mwisho ambay” binadamu anangojea ulimwenguni.
Wahusika wanaokaa na kulała huku wakisubiri kuokolewa ni wa kiubwege. Katika Watingfor Godot, tunapata Madimir na Estragon katika hali duni na ya uhitaji lakini hawatcndi la
kuwanufaisha ila kumngojea Godot, ambaye tunaweza lcumchukulia kuwa mwokozi au Mungu wao. Matumaini ya wahusika hawa yanatumbukia nyongo kwa vile Godot hat^kei na udum wao kunata zaidi.
Hali hii ya kutotenda la maana ila kutegemea misaada na wokovu, inaendeleza imam ya kidhanaishi kuwa maisha ni majaaliwa na binadamu huishi kibahati. Kezilahabi, mmoja wa waandishi tajika wa kidhanaishi barani Afrika anasema:1
Maisha ni mkondo. hakuna kurudi nyuma.
Kama maj i katika mteremko,
Maisha ya mwanadamu huenda mbele kwa kasi sana
62