Ame: Nafsi yako.
Zidi: Nafsi yangu imefanyaje?
Ame: Inajicheka.
Zidi: Labda inajicheka au inatucheka Mimi na wewe Ame: Sasa?
Zidi: Sasa nini?
Ame: Kuhusu Mari
Zidi: Nilimwonesha kasri letu.
Kicheko
cha Mari: Ha, ha, ha. ..
(uk. 24-25)
Vicheko hivi, ambavyo havijulikani vinakotokea vinatumiwa na mwandishi kuwakilisha mtazamo wa mapinduzi ya kimaendeleo ambao unahitaji viongozi na raia kwa ujumla kama Ame na Zidi, wajitolee katika kujijua na kujitambua vyema zaidi iii waweze kuboresha maisha yao. Hala hivyo, vicheko hivi haviwasaidii kurekebisha hali zao. Ni hali inayoendeleza vipengele vya drama ya kiubwege.
4.6 LUGHA NA MAWASILIANO
Wahusika wa kiubwege wanapotumia lugha inayotatiza mawasiliano, wanafanya hivyo kimakusudi iii kudhihirisha kuwa lugha imeshindwa na jukumu lakę la kimawasiliano, inajirejelea yenyewe Mawasiliano, au mazungumzo yanayovunja kaida za kimawasiliano na yasiyo na mantiki mwafaka ni dhihirisho la lugha kujirejelea yenyewe kuwa imeshindwa katika wajibu wake.
Tamthilia za kiubwege hutazamwa kama vitendawili mzunguko, vichekesho vya huzuni, kejeli kwa maumivu, mizaha ya kipumbavu na masihara dhanaishi Ni aina ya michezo inayoafikiana na usemi wa Sigmund Freud3:
92