Wimbo wanaoimba Ame na Zidi katika onyesho la tatu unaendeleza majivuno ya Waafrika Rangi nyeusi inaonewa fahari na wahusika hawa ingawa umuhimu wake haudhihiriki bayana. Ni wimbo ambao mtunzi anautumia baada ya kumsawiri Mari Mari ni mhusika ambaye amekengeuka kiasi cha kudharau na kutotambua mambo na hali ya bara la Afrika, bara lakę. Mari anathamini na kutukuza ya Mzungu Wimbo huu basi unaelekea kuwakashifu Waafrika wanaodunisha hali yao kwa kufuata ya kigeni Ame na Zidi wanaimba:
Tunaimba wimbo huu Wimbo wa fahari na makuu Tunaimba kuisifu rangi hii ya fuu (wanaonyesha ngozi zao)
(uk. 27)
Huu ni wimbo wa kiuhalisia, hauna maudhui ya kiudhanaishi Hali ya Waafrika ambao ni maskini, kutegemea na kufurahia visivyo vyao kama magari, vifaru, mavazi na vyakula, ni dhahiri. Hata hivyo, mwishoni mwa wimbo huu, tunapata miale ya ubwege Taswira ya watu wazembe na wasio na uwezo wa kutekeleza lolote lenye manufaa ila kungojea majaaliwa hubainika. Wanatuambia:
Na kazi, ya nini kazi?
Haina haja kazi!
Ya nini uvumbuzi?
Tu huru: tumejitawala!
Tuna kila kitu kwa fedha zetu Tuvumbue, tuvumbue nini?
Tutawalipa wanaovumbua...
Wanaotuvumbulia (uk. 28)
Ni wimbo unaokejeli Waafrika kwa kujidai kuwa wako huru huku wakiendelea kumtegemea Mzungu Aidha, unatupatia picha inayokaribiana na ya Vladimir na Estragon katika Waiting for Godot. Wahusikia hawa wanasawiriwa kama vibonzo kwa kukaa, kupiga domo ovyo ovyo huku wakimngojea Godot Ni wahusika ambao hawana hata uwezo wa kuvua viatu (uk 9).