Badała ya Ame na Zidi kufanya kazi, wanatumia wakati wao mwingi kulała na kuzungumza. Suala hili la mazungumzo ni muhimu katika fasihi ya kiubwege Wahusika wa kiubwege mara nyingi hujiingiza katika mazungumzo ambayo aghalabu yanazuia uelewano na badała yake kuzua ubishi usio na maana yoyote Hali ya mwandishi kusawiri wahusika hafifu wasioelewana kwa mambo madogo madogo na ambayo hukosa mantiki ya mazungumzo, ni kigezo muhimu kinachoendeleza hali ya ubwege na hivyo hivyo kukuza imani ya kidhanaishi kuwa maisha ni fujo na hayana maana yoyote. Ame na Zidi katika onyesho la kwanza wanabishana kuhusu masuala ya kikawaida kama kuamka, kulała, hali ya kuwa kumekucha, hali ya suruali iliyoraruka makalioni, na hali ya mhogo uliovunda. (uk. 4-5)
Aidha wahusika hawa hutatiza mawasiliano kwa kuingiza hoja ambazo hazina uhusiano wowote na yale yanayokithiri. Mfano suala la suruali kuliwa na panya, au panya kuliwa na suruali, halina umantiki wala maana ya moja kwa moja kulingana na muktadha wa mazungumzo ya wahusika (uk. 5). Hili ni suala la ubwege.
Wahusika hawa ni wazembe na wajinga Ame na Zidi wanajikuta katika hali ya uhitaji mwingi ambayo inawalazimisha kukubali usaidizi usiofaa Misaada wanayopewa haina thamani. Mihogo iliyovunda tunaambiwa imetoka nje Nje hapa panaweza kumaanisha nje ya bara la Afrika; ni jazanda ya misaada mibaya na yenye vikwazo ambayo Wazungu hutunukia Waafrika Tamthilia inaendeleza wazo hili kupitia Ame na Zidi:
Zidi: Ujue cha kuliwa......
Ame: Kinacholiwa.
Zidi: Mhogo wa kuvunda...
Ame: Mpe paka.
Zidi: Hataula Ame: Mpe mbwa.
Zidi: Ataunusa tu ‘ende zake.
Ame: Mpe mbuzi.
Zidi: Labda labda mbuzi aliyekosa majani! (uk. 6)
60