Mbuzi aliyekosa majani ni jazanda ya Waafrika wanaokufa kwa njaa kwa sababu ya ukame na vita vya wenyewe kwa wenyewe Kwa kukosa njia bora ya kujisaidia (majani), hupokea misaada yoyote hata yenye kasoro nyingi na kuifurahia. Hali hii ya wahusika kufurahia vitu vibaya huendeleza imani ya kidhanaishi kuwa ulimwengu hauna wema na binadamu hawezi kupata furaha ya kudumu maishani mwake
Hali hii inaendelezwa vyema kupitia sauti ya redio inayoeleza kuwa:
...Umoja wa Mataifa unaandaa misaada Marekani ishapeleka misaada ya magunia milioni ya sembe na dona... Uingereza imepeleka mitumba na nyama ya kukausha... Ufaransa imetoa madawa ambayo huko hayahitajiki tena. (uk. 35).
Kupokea misaada si tendo baya, lakini kutegemea misaada kila wakati ni ulitima unaochukiza. Ikumbukwe kuwa, Ame na Zidi wana kazi, nchi yao ina rutuba, madini na malighafi nyingine chungu nzima, lakini hawafanyi lolote la maana kurekebisha hali yao ya maisha. Mali yao inapotea tu, wameipoteza kwa ujinga wao Tunaambiwa kuwa kasri lao halina maji, hata tonę moja:
Ame: Tumekuwa tukijidanganya, Zidi Zidi Hivi kweli kasri hili lote halina maji?
Ame: Enh, hamna maji hata tonę moja!
Zidi: Tumekuwa tukijidanganya, Ame!
Ame: Hapana; sikudanganya, Zidi Zidi. Aaaaaa, hunifahamu . . ka... hamkuwa na lolote ila mlitawaliwa na ujinga, uvivu, mapuuza, unafiki, wivu, choyo... humu katika kasri letu ...
Ame: Hapana Mlikuwa na maji na kila kitu humu; ela vimehama...
61