5.2 MAANA YA MAISHA
Kiudhanaishi, maisha ni hatua ya kuelekea kifo. Binadamu pamoja na vitu vyote vilivyomo ulimwenguni vinazungukwa na ubwege, utupu Vitu huzaliwa bila mpango wala sababu Aidha, vitu hivyo vinajidunisha vyenyewe kwa unyonge, na hufa kwa unasibu tu.
Katika kuvitalii vina vya sababu na umuhimu wa kuwepo kwa binadamu ulimwenguni, udhanaishi unatuonyesha dhahiri ombwe lenye giza totoro ambalo huwakilisha uduni na unyonge wa binadamu ulimwenguni. Kile ambacho ni bayana, ni binadamu kukaa tu huku akisubiri kifo Inabainika pia kuwa, binadamu hana uwezo wa kuchagua matendo yake, ila kufanikisha majaaliwa yake. Matumaini ya maisha mema siku zijazo ni maliwazo tu kwa binadamu Sartre (1985:157)3 anasema:
Sisi ni viumbe tuliofungamanishwa kwa ulimwengu - na hicho ndicho kitovu cha matatizo yetu yote.
(Tafsiri yetu)
Njogu na Chimerah (1999:75) wanaeleza kuwa ubwege ni maumivu ya kifalsafa kuhusu maisha ya binadamu yasiyokuwa na mwelekeo na yaliyotamauka Hii ndiyo tasnifu ya maisha kufuatana na maandishi ya kibwege. Kwa wahusika wa kiubwege, maisha ni ruiya tu Wahusika hawa hujiepusha na kutenda, na badała yake huketi tu na kuzungumza. Hii ni sanaa ya kupotea kwa nafsia, na kwao wokovu haujibainishi. Wahusika hawa hawatendi la maana kwa sababu wokovu ni jambo linalowazidi uwezo Kwao, maisha ni kama ndoto, ni kama mazigazi ndiposa Ame katika Amezidi. anasema:
... tunafurahi na mbele yetu mazigazi.. mazigazi... mazigazi... nini basi kama si ndoto ya kujidanganya tu?
(uk. 83)
101