9058009937

9058009937



Binadamu anaugua kutokana na maambukizo ya huzuni; amefanywa bubu kutokana na kuporomoka kwa lugha na mantiki, na anaweza tu kuipaaza sauti yake hoi kwenye ombwe lisilo na furaha (Tafsiri yetu)

Kawaida, lugha ya sanaa ya kiubwege hukwamiza mawasiliano. Njogu na Chimerah (1999:75) wanaeleza kuwa lugha ya sanaa ya kiubwege hairahisishi mawasiliano; badała yake hukinzana na jukumu lakę la mawasiliano. Ugumu wa kuishi unaashiriwa na ugumu wa mawasiliano katika sanaa ya aina hii. Hii ni sanaa inayoonyesha uvunjaji wa kaida za lugha, na inasawiri mdundo wa uvunjikaji wa lugha inavyotumiwa kwa minajili ya mazungumzo mengi ya kidhahania; kwa mfano, uhusiano wa kifo na uhai, kulała na kuamka.

Hali hii ndiyo hubainika katika tamthilia ya Amezidi Katika onyesho la kwanza, Ame na Zidi wanajadiliana:

Ame: Suruali au ghuba?

Zidi: Suruali.

Ame: Suruali imeliwa na panya.

Zidi: Panya ameliwa na suruali... i    na nyani haoni ghubaye.

Ame Suruali imeliwa na panya na hapa hapana nyani...

Zidi: Aha...unasema mhogo uliovunda?

(uk. 5)

Haya ni mazungumao yasiyokuwa na mantiki wala maana yoyote. Wanazungumza juu ya suruali, kisha ghafla kuingilia mhogo bila kutuonyesha mwingiliano wowote. Haya ni mawasiliano ya kiubwege, ambapo lugha na kaida zake huvurugwa iii kuashiria hali ya maisha yenye fujo.

93



Wyszukiwarka

Podobne podstrony:
Binadamu anaugua kutokana na maambukizo ya huzuni; amefanywa bubu kutokana na kuporomoka kwa&nb
Hali hizi, hujenga na kuendeleza picha ya mazingira ya kiubwege, yaani ulimwengu unaomtesa binadamu,
5.2 MAANA YA MAISHA Kiudhanaishi, maisha ni hatua ya kuelekea kifo. Binadamu pamoja na vitu vyote vi
Hali hii humpatia binadamu picha halisi juu ya maisha yake yasiyo na utaratibu wowote ulimwenguni. M
Aidha, tunapata ‘Wimbo wa Mzee’, wimbo ambao sawa na dondoo kutoka Kilio cha Haki, unapitisha haja y
skanuj0010 (67) • Wektory Współrzędne wektora AB, który przesuwa punkt A na punkt B: AB = [xB-xA,yB-
skanuj0010 (67) • Wektory Współrzędne wektora AB, który przesuwa punkt A na punkt B: AB = [xB-xA,yB-
Untitled Scanned 41 (X Obouc^e toLtowtfe ópocarufcouśj /na " iO~ 155 Bil/ya qo. %o -- 9,06 kWm
skanuj0022 Ayf ^ Ą/l ć.- bĄ ^ i/l 6- 1/1 nA PA <- i A ćr~ ?/! 4s1 /- W ł- YA *- 2A 4A  
SPOK NOCY Na dobranoc przesyłam ci całusków moc na słodkie sny całuski trzy i jeszcze dya
71 (179) yĄ K ły i [o- miji <1 U.#V
80 (83) id PRZEKROJU NA RZUCIEcj yk/YA/r <73 Wż 77 u* \v -NnN %H—h + H- + + + + + + +
skf82 bmp Vł i-ft t Sfl/i i ĘtJ/t -P :0 , ~yA^v-:i5:NA ■pi —- ij 4 •
Mtindo wa tamthilia zetu umetokana na ule wa fasihi ya Kiingereza ambayo ililetwa kwetu na elimu ya
4.7 PLOTI Ploti kwa kifupi ni ule msuko wa vitushi na namna vitushi hivyo vinavyosababishana; ni seh
Haya ni maisha ya kukatisha tamaa kwa umma Ni maisha ambayo hayatoi matumaini kwa watu wapenda maend
Kiudhanaishi, maisha ya binadamu husawiriwa kama fujo Hali hii hubainika kupitia shughuli mbalimbali

więcej podobnych podstron