Hali hii humpatia binadamu picha halisi juu ya maisha yake yasiyo na utaratibu wowote ulimwenguni.
Matukio ya tamthilia za kiubwege hubainika kimzunguko. Matumizi ya duara ni kigezo muhimu katika aina hii ya drama Esslin (1961:365) anaeleza:
Nyingi ya tamthilia za kiubwege huwa na muundo wa kjduara, ambapo zinaisha vile ambavyo zilianza; zingine huendelezwa kwa hali iliyotangulia. (Tafsiri yetu)
Hali hii ndiyo hudhihirika katika tamthilia za Beckett na Ionesco. Katika End gamę (1958), hamu ya Clov kutaka kutoka nyumbani kwa Hamm inajitokeza kuanzia mwanzo hadi mwishoni mwa tamthilia, kwa vile Clov haondoki. Katika tamthilia nyingine ya Beckett Waiting for Godot (1956), wahusika Estragon na Vladimir wanaendelea kumngoja Godot mwanzoni na pia mwishoni mwa tamthilia Eugene Ionesco katika Rhinoceros (1959) anatupatia hali ambapo mhusika Berenger anaendelea kuzidiwa na woga wa kubadilika kuwa Rhinoceros. Hali hii pia inabainika katika The Lesson ambapo wahusika, Professor na Pupil wanabadilika kadiri mchezo unaposonga mbele hadi kiwango cha mwanafunzi, Pupil, kuzidiwa kabisa na hapo kuuawa na Professor.
Tamthilia hizi ni kiwakilishi cha hali ya fujo inayojibaini ulimwenguni. Wahusika wa tamthilia za kiubwege ni vibonzo. Mazungumzo yao hayana umantiki na hivyo mawasiliano hutatizika Wahusika hawa hawawakilishi sifa halisi za binadamu bali huwakilisha dhana za kidhahania. Anderson (1972:2) anafafanua hali hii anaposema:
Wakati mwingine wahusika hawa hubadilisha hali zao, mazungumzo yao yamejaa ukinzano, hukataa kukubali yaliyomo ulimwenguni na badała yake kuamini matukio ya kidhahania.
Maelezo yao juu ya hali na dhana mbalimbali hukosa maana (Tafsiri yetu)
30