Kiudhanaishi, maisha ya binadamu husawiriwa kama fujo Hali hii hubainika kupitia shughuli mbalimbali za binadamu ambazo hazidhihirishi utaratibu wowote. Matendo ya binadamu maishani ni shaghalabaghala kwa vile kila mtu hutenda atakavyo na hashurutishwi na yeyote, si hata Mungu. kutenda atendavyo au kusema asemavyo. Hali hii hubainika katika Amezidi tunapowapata wahusika wakitenda watakavyo mfano kutoenda kazi. kutegemea misaada, kuiba mali ya umma na kulała; na kusema wayapendayo mfano kuliita pango lao kasri na kulipamba kwa utajiri mwingi wa kindoto.
Aidha, katika onyesho la nne, tunapatiwa mandhari ya darasani, ambayo huendeleza wazo la maisha kama fujo. Wanafunzi ni zogo, mwalimu ni kibonzo asiyeelewa kazi yake na amekiuka kaida za ualimu; sauti ya redio inasikika katikati ya kipindi na kuna kucheka na kulia darasani na kadhalika. Kweli haya ni mazingira yasiyopendeza na yanayoendeleza hali ya maisha kama fujo.
Waandishi kadhaa wameshughulikia wazo hili la maisha kama fujo Kezilahabi katika Dunia Uwcmja wa Fujo (1975:92), amesawiri dunia kama uwanja wa fujo. Inabainishwa kwamba, kila mwanadamu ameumbwa kufanya fujo zake halafu ajiondokee ulimwenguni. Uzito wa fujo hutofautiana kwa vile kuna watu ambao hufanya fujo zaidi ya wengine. Maisha hayana lolote la maana ila kufanya fujo huku ukingojea kifo.
Uhusiano kati ya kifo na maisha ni suala la kimsingi katika tapo la kiubwege Kiudhanaishi maisha ni kufa pole pole. na kifo si jambo la kumshughulisha binadamu kwa vile ndicho hatua ya mwisho anavoisubiri. Baada ya kuishi kiubwege. Ame na Zidi wanakufa. kifo cha maumivu na raha
Wazo la chanzo cha maisha ya binadamu na kifo Iimemsumbua na kumpumbaza binadamu kwa muda mrefu Binadamu ametumia wakati wake mwingi kufikiria juu ya suala hili bila kupata ukweli. Maisha ya binadamu ni mithili ya kitendawili chepesi, lakini kwa vile binadamu ameamua kutofikiria, ameshindwa kukitegua. Kuhusu hali hii, lgnące Lepp-*, anasema:
108