Tamthilia katika onyesho la kwanza, inajaribu kueleza hali na uhusiano wa kiuchumi baina ya bara la Afrika na la Ulaya. Ame na Zidi wanajadiliana juu ya mihogo iliyovunda, isiyofaa na jinsi ya kuitayarisha iii iweze kulika Baadaye tunawaona wakishindwa kuikata na kuichoma, na hivyo kulazimika kuila tu kinyama.
Maisha ya binadamu kulinganishwa na ya wanyama ni kigezo cha ubwege. Mwanadamu amepotea njia na kujitoma katika ulimwengu wa kinyama Haya ni maisha mabaya, machafu mithili ya kiumbe wa kiubwege Wanyama hawana uwezo wa kuboresha maisha yao sawa na Ame na Zidi ambao tunaambiwa hawana kisu wala kibiriti ambacho kingewasaidia kutayarisha chakula chao (uk 10-11)
Hata hivyo, hali hii ni fumbo kuhusu hali mbaya ya biashara kati ya mataifa ya Ulaya na ya Kiafrika Waafrika, inabainika, wanahitaji vitu vingi zaidi kutoka Ulaya huku nchi za Kimagharibi zikisawiriwa kama zilizoendelea sana na kujitosheleza kimahitaji. Aidha, Waafrika wanasawiriwa kama watu wajinga ambao hawataki kufikiria na kujizatiti kuvumbua vitu vyao Kwao, muhimu ni kulała, kuzembea kazi na kumtegemea Mzungu kwa yote. Zidi anasema:
Kwanza yanaumiza kichwa, pili, utafikiri kipi wewe Mwafrika ambacho Wamarekani, Waingereza, Warusi, Wafaransa na Wajerumani hawajakifikiria? Tatu, si vipo tu vitu vyenyewe duniani vimeenea? Na sisi tunanunua tu Huu ulimwengu wa biashara ati! (uk. 10)
Hii ni hali inayobainika bayana hata hapa nchini mwetu, ni hali ya kiuhalisia Ubwege urno katika maisha ya Waafrika (Ame na Zidi). Wahusika hawa hawana uwezo wala nia ya kutekeleza wajibu wao wa kikazi licha ya kupatiwa mazingira yenye rutuba, na malighafi muhimu.
37