Katika onyesho la nane, Ame na Zidi wanakubali kuwa mazingira ya maisha yao ni duni lakini lewa vile wameyazoea, yamekuwa kama kasri Kwao harufu mbaya ni uturi. Wanasemezana
Zidi: (Anaziba pua) MmmfF
Ame: Nini?
Zidi: Harufu! (Anaziba pua)
Ame: Nini?
Zidi: Uvundo! (Anaziba pua)
Ame: La, pana uturi hapa9
Zidi: Uturi - mzoga!
Ame: La, mzoga-uturi (uk. 64)
Mohamed, katika Ameiidi pia amewapatia wahusika wake vifaa duni kama kibenza na vijiti (uk. 10); kupekecha moto badała ya kutumia kibiriti (uk. 11), kiserema, mavi ya ng ombe na samadi (uk. 38) na kadhalika. Vifaa na hali hizi huchora mazingira ya kuchukiza yasiyomsaidia binadamu kuishi katika furaha, bali huendelea kumdhoofisha kifikira na kimaisha.
Kuna matumizi ya mandhari na dhana zinazosheheni ishara za giza na mwangaza Gtza ni ishara ya woga. Mazingira yenye giza huogofya na hukatisha tamaa kwa binadamu anayetaka kuona mbele. Hali hii husaidia kufafanua maisha ya binadamu ulimwenguni Binadamu amegubikwa na giza totoro na ni sharti atafute mwangaza iii aweze kugundua ukweii wa kuweko kwake ulimwenguni. Mohamed ametumia neno GIZA kama kimalizio cha maonyesho vake Amedhamiria kubainisha utata wa maisha ya binadamu, maisha ambayo hayana mwelekeo na yanayoendelea kudidimia Katika onyesho la kwanza, tunaambiwa:
Spotilaiti inafuata wahusika (uk. 4)
70