9365206656

9365206656



Nlohamed anatumia mbinu ya mhusika ndani ya mhusika katika tamthilia ya Amezidi. Ame na Zidi wanabadilikabadilika na kuchukua nyadhifa mbalimbali kulingana na mahitaji ya mtunzi. Kwa mfano Ame anakuwa Mari katika onyesho la tatu, Mwanafiinzi katika onyesho la nne huku Zidi akiwa Mwalimu wake. Katika onyesho la tano, Ame ni bosi na Zidi ni msaidizi wake. Hali hii hubainika katika kazi za kiubwege chambilecho Anderson (1972:2) anayesema:

Wakati mwingine wahusika hawa hubadilika hali zao, mazungumzo yao yamejaa ukinzano; hukataa kuamini yaliyomo ulimwenguni na badała yake kukubali matukio ya kidhahania Maelezo yao juu ya hali na dhana mbalimbali hukosa maana.

(Tafsiri yetu)

Kigezo cha kutozingatia yaliyomo na kuamini ya kufikirika kinadhihirika wazi katika Amezidi Ame na Zidi wanaishi katika ulimwengu wa kindoto Badała ya kukubali hali yao duni ndani ya pango, wanaota na kuamini juu ya kasri lenye fahari Hii ni hali ya wigo bubu, mbinu inayoendeleza ubwege wa wahusika hawa.

Kwingineko, Ionesco katika The Chairs, The Lesson, na Rhinoceros anasawiri wahusika wanaobadilika badilika na ambao wanaamini vitu na mambo ya kidhahania. sawa na wenzao katika Amezidi.

Ajdha. katika Amezidi, tunakumbana na wahusika ambao hawajui watokako wala wanakoelekea Wanajigamba kuwa wao ni matajiri huku wakiendelea kuhitaji na kupokea misaada Ame na Zidi wanajua kwamba misaada wanayopata ni mibaya, imevunda lakini bado wanaipokea na kuitumia Hawa ni wahusika wapumbavu waliochanganyikiwa na wanaofurahia uvundo. Ni wahusika wa kibwege.

67



Wyszukiwarka

Podobne podstrony:
Katika onyesho la nane, Ame na Zidi wanakubali kuwa mazingira ya maisha yao ni duni lakini lewa vile
1.7 YALIYOANDIKWA KUHUSU SOMO HILI Tamthilia ya Amezidi kama ambavyo tumetaja awali, imeshughulikiwa
Kundi la kwanza lilijikita zaidi katika matumizi ya yaliyomo katika tamthilia kudhihirisha dhana ya
Wahusika wa kiubwege hukosa historia. Katika tamthilia ya Amezidi, wahusika tunaopewa hawana ukuaji
Badała ya Ame na Zidi kufanya kazi, wanatumia wakati wao mwingi kulała na kuzungumza. Suala hili la
Tamthilia ya Amezidi inabainisha mazingira ya kibunilizi yenye ishara mbalimbali za kiuasilia Onyesh
Wimbo wanaoimba Ame na Zidi katika onyesho la tatu unaendeleza majivuno ya Waafrika Rangi nyeusi ina
skanuj0009 (405) IM..    jg a wv) xU&. -4 i- ?ya>lo-1 fioŁ-HyulA 1 iii -i- łud
skanuj0010 (67) • Wektory Współrzędne wektora AB, który przesuwa punkt A na punkt B: AB = [xB-xA,yB-
skanuj0011 (57) • Trójkąt Pole trójkąta ABC o wierzchołkach A = (xa, yA), B = (xb, yB), C = (xc,yc),
skanuj0033 (45) Multifidi 06D/Vu Sllye^ot-YĄ-

więcej podobnych podstron