Wahusika wa kiubwege hukosa historia. Katika tamthilia ya Amezidi, wahusika tunaopewa hawana ukuaji unaofuata misingi ya kiuhalisia Ingawa kuna chembechembe za historia hasa kupitia mzee na wimbo wake, wahusika wakuu Ame na Zidi wanajitokeza tu kama mapacha, vibonzo wa kutumika kutekeleza majukumu fulani tu. Zaidi ya hayo, hatuonyeshwi asili yao, umri wao wala kazi zao kikamilifu.
Kuhusu suala la utendaji, wahusika wa kibwege hawapatiwi nafasi ya kutenda au kutekeleza mambo ya maana Njogu na Chimerah (1999:75) wanaeleza kuwa:
Wahusika wa kibwege hujiepusha na kutenda, na badała yake huketi na kuzungumza tu.
Ame na Zidi hawafanyi lolote la maana kujinufaisha au kuboresha hali yao duni. Ni wahusika waliokwama kwenye shida nyingi zikiwemo umaskini, ukosefu wa ujuzi na elimu, na magonjwa mabaya, lakini hatuwaoni wakijaribu kujinasua kutoka kwa minyororo ya uduni inayowazunguka Wanalofanya aghalabu ni kulała tu. Tunasoma:
Ame: Na kwa nini mtu apende kazi? Mungu yupo na ardhi ipo... na ardhi yenyewe bikra ikidondoka mbegu tu imeshaota! Ukiatika kambu za migomba kesho utakula ndizi: na hata mwaka mzima ardhi inakubali tu, haichoki. Wewe kula tu na kulała! Ah, hata Mungu alifanya kazi siku saba, kisha akapumzika na wewe ulilala siku ngapi vile?
Zidi: Siku tisa kama wewe!
Wahusika wa namna hii, ambao hawatendi lolote la maana ni sawa na binadamu wa kidhanaishi anayeishi tu huku akisubiri kifo
59