Inabainika kuwa. Mohamed ameathiriwa na mtazamo wa kiubwege Kiubwege, wahusika hawaendelezwi kihistoria Wahusika huonyesha ubatili wa maisha ya binadamu katika mazingira dhalimu yanayokatisha tamaa. Pengine Mohamed ameiga mtindo wa waandishi kama Samwel Beckett, Waitingfor Godot, Esid gamę na Eugene Ionesco, The I.essoti, The Chairs na The Ki ller.
Irungu (1999) anaeleza kuwa maisha ya binadamu ni safari ya kuzunguka kwenye duara Katika Amezidi wahusika wanazunguka kwenye shida ya umaskini na uhitaji wa misaada. Hali hii pia hubainika katika kazi za kiudhanaishi kama za Kezilahabi. Mwandishi huyu katika Mzingile (uk. 5) anatumia sitiari ya sayari na jua kuonyesha jinsi maisha ya binadamu yalivyo. Sayari huwa mbioni kulizunguka jua, vivyo hivyo binadamu huwa mbioni kuusaka ukweli na uhalisi wa maisha yake, na ni kama kwamba huwa mbioni kulizunguka jua lakę lisiloonekana Maisha ni mzunguko, ni duara. Binadamu amefumbwa macho ndiposa anatafuta kitu kilicho wazi, ukweli wa maisha yake ulimwenguni.
Katika Amezidi, Mohamed amesawiri wahusika wanaoishi katika pango Pango ni ishara ya mzunguko. Ndani ya pango sawa na ndani ya shimo hamna mwangaza. Hivyo basi, wahusika Ame na Zidi huzunguka duara lao ovyo ovyo kama vipofu Hii ni hali duni ya maisha kuashiria mateso na utupu wa binadamu ulimwenguni.
4.8 HITTMISHO
Sura hii sawa na ya tatu imemulika vipengele muhimu hasa vya kifani ambavyo hufanya tamthilia ya Amezidi kuwa na mwelekeo wa kiubwege. Aidha tumebainisha kuwa tamthilia ya Amezidi inaweza kufananishwa na tamthilia za ubwege za Kimagharibi mfano Waiting for Godot yake Samuel Beckett na The Lesson yake Eugene Ionesco.
Amezidi inawakilisha ubwege wa Kiafrika na kwa kiasi inatofautiana na tamthilia zingine za ubwege Ingawa wahusika wake wanakatisha tamaa wanasawiri chembechembe za matumaini.
97