Aidha, inabainika kuwa hadithi ya watu wanaoishi katika ulimwengu wa kidhahania wa kufikirika tu inafanana na ngano ya pango la Plato4 Kwa mujibu wa Ayi Kwei Armah, ngano ya pango la Plato inatamba hadithi ya watu waliofungwa na minyororo na kuishi katika kiza cha pango katika kipindi cha maisha yao yote. Ilitokea kuwa, mfungwa mmoja alipata nafasi ya kutoka nje ya pango na akawahi kujionea uzuri na utamu wa jua. Mfungwa huyo aliporudi pangoni, aliwaelezea wenzake juu ya mwangaza na ubora wake lakini hakuna aliyemwamini.Mwenye kuona mwangaza alidharauliwa na kuitwa mzushi na mwehu .
Ngano hii imetolewa kufundisha jamaa kuwa watu wanaoishi katika mazingira na hali tofauti za kilimwengu huwa na maono tofauti. Wale wanaoishi katika ulimwengu finyu kimawazo hawana uwezo wa kufikiria na kuona mambo yaliyoko nje ya duara lao finyu.
Hali hii ndiyo hubainika katika tamthilia ya. Amezidi. Wakazi wa nchi ya Amezidi wamekubali ulimwengu wao duni na kuukabidhi maana za kipekee na ambazo hazieleweki nje ya muktadha wao. Pango, kwao ni kasri zuri lililosheheni ubora wa kisasa. Katika tamthilia hii, pango linapatiwa maana za aina yake Kadhia nyingi zinazohusu maisha ya raia wa Amezidi zinaigizwa pangoni Mazingira haya ni ya kuchukiza na yana nia ya kuashiria uduni.uchafu na maisha yasiyokuwa na thamani- maisha ya Mwafrika.
Mohamed anabadilisha badilisha pango lakę na kulipa mandhari tofauti ya kimawazo Taswira ya pango machoni mwa wasomaji hugeukageuka kutegemea madhumuni ya mwandishi Onyesho la kwanza na la pili kwa mfano huashiria uasili wa Mwafrika. Pango linaashiria hali isiyobadilika ya maisha ya bara la Afrika. Ni bara ambalo halijaendelea kiteknolojia wala kurutubisha historia ya wakazi wake. Tunaambiwa :
Tendo hili lote linatokea ndotoni mwa Ame
na zidi ...pahaia ni palepale pangoni!
Aidha, tunaambiwa kuwa,
(kaketi chini kwenye majani ambayo ni godoro
lakę. Anamtikisha :idi.)Aimka bwana. siku ngapi zirnepita9
(uk 12)
76