Kundi la kwanza lilijikita zaidi katika matumizi ya yaliyomo katika tamthilia kudhihirisha dhana ya ubwege Waandishi hawa, walitumia muundo wa kiakili kusawiri hali duni, ya kiubwege ya binadamu Tainthilia zao hueleweka na hubainisha maana kupitia tendo la kufikiri. Kazi zao za awali hazibainishi ubwege kamili Kwa mfano tamthilia The Kiisunderstanding na Caliąula za Camus, zina ploti nzuri inayofululiza Lakini kazi zake za baadaye kama Siatę of Siege na The Jus! Assassins zina vipengele vingi vya kiubwege ambavyo vimeimarishwa. Kwa mfano, ukosefu wa muwala na umantiki katika ploti na usawiri wa wahusika ni bayana
Waandishi wa kundi la pili hutofautiana na wa kwanza kwa vile tamthilia zao zimepevuka zaidi kiubwege. Kazi zao huonyesha picha halisi ya kukata tamaa kwa binadamu kutokana na hali duni na maisha yenye mateso katika ulimwengu katili usiomjali. Tamthilia za Beckett Waiting for Godot na End gamę pamoja na za Ionesco The Lesson, The Chairs, Rhinoceros na The Killer kwa mfano ni kazi ambazo zimeafiki sifa muhimu za ubwege, kama ambavyo tumekwisha zitaja na kuzifafanua Tamthilia za kundi hili la pili hutumia vigezo vya yaliyomo na mtindo katika kupitisha maana. Hawategemei yaliyomo peke yake kama kundi la kwanza. Kuhusu hali hii, Esslin (1961:6) anasema:
... Sartre au Camus huelezea yaliyomo kwa kutumia kaida za kale lakini drama ya kiubwege ya kisasa hupiga hatua mbele katika jaribio la kupata muumano kati ya dhana zake za kimsingi na maumbo mbalimbali ambayo huelezea dhana hizi.
(Tafsiri yetu)
Ingawa kuna haya makundi mawili, drama ya kiubwege kwa ujumla huongozwa na wazo la kuweko kwa binadamu ulimwenguni, maisha yake duni na yasiyo na maana katika ulimwengu huo katili na wa kukatisha tamaa. Kitchin (1966:31) anathibitisha wazo hili anaposema kuwa haja kubwa ya drama ya kiubwege ni kuweko kwa binadamu katika hali ya kukata tamaa na isiyo na maana ulimwenguni.
32