Kuchanganyikiwa kwa mfumo wa elimu ya Kiafrika unabainika zaidi, tunapopatiwa sauti ya redio Mazingira ya darasani, ghafla yanabadilika na tunasikia redio ikitoa matangazo Sauti hii ya redio inaashiria utupu wa nchi ya Amezidi. Mtunzi anaitumia kuikejeli zaidi elimu ya bara la Afrika. Nchi nyingi, redio inasema, bado zinaendelea kuhitaji na kupokea misaada kutoka ng’ambo, misaada ambayo haifai Nchi hizi zina wasomi wengi, na inashangaza kuwa zinatumia misaada na ruzuku zisizofaa Ni dhihirisho la uduni wa elimu ya nchi hizi, ni elimu inayokatisha tamaa kwa vile haisaidii viongozi na raia kutambua kwamba bado wananyanyaswa na nchi za Kimagharibi. Afrika imekuwa ghala la kutupia uchafu wa Kimagharibi kama madawa yasiyohitajika, mitumba, na nyama mbovu.
Ubwege unaendelezwa zaidi tunapopata mwalimu na wanafunzi wamelala huku redio ikitoa taarifa Mwalimu anasema:
Barabara. ajuitabasamu Dakika tano za kulała...tunza yenu! (Wcmalala na mwalimu wao juu ya meza zisizokuwepo).
(uk. 35)
Nani anapatiwa ujumbe huu wa redio? Ni dhahiri kuwa wasomi wamefumba macho yao na kuziba masikio yao iii wasisikie na kugundua uozo wao; wametafuta njia za kukwepa lawama. Camus (1953:11) anaeleza:
Tunaishi katika kipindi chenye uhalifu mwingi Wahalifu tunaoshuhudia sasa si watoto dhaifu bali ni watu wazima ambao wamepata njia ya kujitoa lawama kwa kutumia ujanja Wanatumia falsafa. ambayo pia inaweza kutumiwa kwa lolote, hata kugeuza wauaji kuwa mahakimu (Tafsiri yetu)
49