9365206666

9365206666



Mohamed amefuata mtindo wa watunzi wa drama ya kiubwege Hawa huchora wahusika, wanaosawiri na kuendeleza mazingira ya maisha ya kinyama. Wahusika wao kwa kiwango kikubwa hushabihiana na wanyama kitabia na kivitendo Katika Amezidi, Ame na Zidi hula mihogo iliyovunda na mibichi kama wanyama Tunawaona wakitumia kucha zao kuumenya mhogo:

Ame: Kwani kucha huna9 Turnia kucha bwana ...

Zidi: Haya (anamwendea na kumpa ile mihogo miwili), imenye kwa kucha basi ..

Ame: Aaaa, hata kumenya kwa kucha żako umeshindwa. .. (anamenya mhogo kwa kucha na kisha...).

Huu mmoja niliokwisha umenya unatosha Menya huo wako sasa!

(uk. 11)

Aidha, wahusika hawa hula nyama mbichi na iliyooza mithili ya wanyama wa mwituni:

Zidi: Njaa!

Ame: Njaa!

Zidi: Una meno?

Ame: N’na meno!

Zidi: Tuwe simba basi.

(wanalitafuna paja la nyama mbichi iliyooza!)

(uk. 72)

Haya ni mazingira ya kiuhayawani, na yenye nia ya kubainisha uduni wa maisha ya binadamu. Tofauti kati ya binadamu na wanyama katika mtazamo wa kiubwege ni nyembamba mno Hali hii hupingana na madai ya kuweko kwa jamii ya binadamu yenye ustaarabu wa kimaisha kutokana na maendeleo ya kiviwanda.

72



Wyszukiwarka

Podobne podstrony:
2.5.5 DRAMA YA KIUBWEQE 0ARąN! AFRIKA Uandishi wa drama ya kiubwege n; mpya katika eneo hili la Afri
Mtindo wa tamthilia zetu umetokana na ule wa fasihi ya Kiingereza ambayo ililetwa kwetu na elimu ya
Kuchanganyikiwa kwa mfumo wa elimu ya Kiafrika unabainika zaidi, tunapopatiwa sauti ya redio Mazingi
wa shule ya upili ya Kegochi, Irene Moraa, Gladys Nyaboke, Carolyne Bochaberi, The 3 Akeyas, Tom Mog
71510 zad2 (12) Z VCotu^Vaya^_ ^ joJodiU> kA&VA^ W*M^ ^^vu^ónjjruj.c^O WA ^od^Ya^e. .OcHoya u
13 -15 rifr wa 2117 SZANOWNI CZYTELNICY ZAPRASZAMY DO WYPEŁNIENIA KUPONU NA NAJCIEKAWSZY ARTYKUŁ NU
Obraz (1375) ^^v^NS^Wa.Ort AsiM£>vu :y*QggNa>U<U- Vsl. dQcl t NA/)^J>Wisj jJt
kama kazi ya kiubwege Ubwege ni tapo la kifasihi linalofuata falsafa ya udhanaishi Mwingiliano huu k
kama kazi ya kiubwege Ubwege ni tapo la kifasihi linalofuata falsafa ya udhanaishi Mwingiliano huu k
Hali hizi, hujenga na kuendeleza picha ya mazingira ya kiubwege, yaani ulimwengu unaomtesa binadamu,
Wimbo wanaoimba Ame na Zidi katika onyesho la tatu unaendeleza majivuno ya Waafrika Rangi nyeusi ina
676ee5d9e49233121660530be338d2ed A r i. ^ v A r ▼ v A- W /WA V Łv^ rA* rAT*yA
mmBgt yĄ
4.7 PLOTI Ploti kwa kifupi ni ule msuko wa vitushi na namna vitushi hivyo vinavyosababishana; ni seh

więcej podobnych podstron