Hali hizi, hujenga na kuendeleza picha ya mazingira ya kiubwege, yaani ulimwengu unaomtesa binadamu, wenye fujo, na unaokatisha tamaa
Licha ya tamthilia kutuchorea mazingira ya kiuchafu na ya kuchukiza, kawaida ya drama ya kiubwege, hapa na pale hutuonyesha hali ambazo zinapendeza na kuvutia. Katika onyesho la pili, pango ambalo Ame na Zidi wanalitazama kama kasri, kwa kiasi kikubwa linatupatia picha ya kuamini kuwa ni kasri kweli. Mawazo ya mazingira yenye uchafu, mbu, mafunza na giza yanatoweka Mtunzi pia analipamba kasri vilivyo. Ndani mule kuna zulia kutoka Iran, meza ya kahawa, makabati ya vitabu, mabakuli ya fedha, TV na video, simu ya rangi ya maziwa, na kadhalika
Aidha, mwandishi amerembesha pango hili kwa kuwapa wahusika wake fikira za umilikaji wa magari ya fahari kama Benz na BMW. Zidi anamwambia Mari:
Gari lipo nje . hukuliona hapo ulipopita?
Na vitu vyako vyote vimo ndani ya mabegi, ngoja nikakutolee.
(uk.23)
Zaidi ya gari, kuna watumishi, vyakula vizuri na vinywaji vya kizungu kama Champagne, Beer, Vodka, Whisky na Brandy. Mazingira kama haya hukiuka misingi ya kiubwege.
4.3.1 PANGO
Sehemu kubwa ya mchezo wa tamthilia ya Amezidi inaigizwa pangoni Pango ni taswira muhimu ambayo mwandishi ametumia kuendeleza madhumuni yake Mohamed ametumia pango kama mandhari ya mchezo wake katika maonyesho manane
Matumizi ya pango katika kazi za kifasihi hayakuanza leo. Waandishi kadhaa wamewahi kutumia dhana ya pango kuonyesha mandhari ya kazi zao Katika tamthilia ya Mashelanił Hussein ametumia pango kuwamba maudhui ya saikologia ya ukoloni na pia ukoloni mamboleo.
75