4.7 PLOTI
Ploti kwa kifupi ni ule msuko wa vitushi na namna vitushi hivyo vinavyosababishana; ni sehemu muhimu ya tamthilia Ploti nzuri, aghalabu hubainika pale ambapo kuna migogoro, na mgogoro mmoja husababisha mgogoro mwingine, na mivutano hiyo ndiyo inayosukuma mbele tamthilia hadi kufikia upeo wa juu.
Tamthilia za ubwege hupuuza kipengele cha ploti. Kazi hizi hukosa migogoro ambayo tunaweza kusema kuwa imejengwa na kusuluhishwa Hivyo basi ni vigumu kubainisha kilele cha kazi ya kiubwege Kile ambacho hubainika katika tamthilia za kiubwege ni mzunguko wa matukio Maisha ya binadamu huwa ni tendo la kuzunguka duara lile lile bila kusonga mbele
Waandishi wa tamthilia za ubwege huashiria hali hii kwa kutoa ploti mzunguko. Badała ya mtiririko wa vitushi kama ilivyo kawaida ya tamthilia za kiuhalisia, sanaa hii ya kiubwege huipa hadhira mpangilio wa kauli na taswira zinazoingiliana na kushajiishana6
Katika Ameztdi, Ame na Zidi wanajihusisha na vitendo ambavyo vinawafanya wategemee na kusubiri misaada Kusubiri huku na kutegemea huku kwa misaada ndicho kigezo cha maana kinachozunguka matendo yao Hatuoni vitushi vikisababishana bali matendo yanaendelea na kurudi pale pale yalipoanzia; ni mzunguko wa matendo.
Hali hii ndiyo hubainika katika tamthilia ya Beckett, Wcutingfor Godot Tunapatiwa mabwege wawili Vladimir na Estragon ambao hawatendi lolote la maana ila kukaa chini ya mti wakimsubiri Godot Kusubiri huku kunatawala tamthilia nzima kwa vile hadi mwishoni, bado wahusika wanaendelea kumtarajia Godot, ambaye pengine atawaokoa kutoka kwa changa walilomo. Godot katika Wattmg for Godot ni sawa na wafadhili katika Amezidi ambao wahusika wanawasubiri wawape misaada ingawa misaada hiyo haifai matumizi yao Haya ni maisha ya mzunguko na ambayo yanaafikiana na mtazamo wa kiubwege chambilecho Esslin (1961:365):
95