Haya ni maisha ya kukatisha tamaa kwa umma Ni maisha ambayo hayatoi matumaini kwa watu wapenda maendeleo, na ambao wanataka kuboresha nchi yao maskini Ame na Zidi wanategemea misaada badała ya kutumia malighafi yao kujitegemea Misaada wanayopewa haifai na hata hawajui kama wataendelea kupatiwa. Haya ni maisha mithili ya ajali asemapo Greene (1960:7):
Binadamu ni ajali, hali yake haina utaratibu na muhimu zaidi ulimwengu umeumbwa kwa hali ya usahaulifu.
(Tafsiri yetu)
Katika onyesho la tisa, Ame na Zidi wanapanga sherehe ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwao Wanatumia pesa nyingi za umma kukumbuka siku ya uhuru wao, siku ambayo hawaelewi umuhimu wake (uk. 75). Wanatumia shilingi milioni arobaini na kualika wageni wengi Tunaambiwa:
Ame: Lakini sherehe ya shilingi milioni arobaini na kualika wageni wapatao laki nne itakuwa sherehe kubwa kwa siku ya kuzaliwa tu...
Zidi: Wewe namna gani bwana, siku ya kuzaliwa unaiona ndogo ..? Watu waliitungia mashairi na nyimbo...
(uk 74)
Ruhumbika (1983:1) anapinga hali hii ya viongozi kuchukua muda mrefu kupanga sherehe kubwa na zisizokuwa na manufaa. Kwake, huo ni utumiaji mbaya wa pesa au mali ya nchi. Kejeli ni kwamba, Ame na Zidi wanasherehekea siku ya uhuru wao, na bado wanaendelea kuwategemea wahisani kwa misaada. Huu si uhuru kamwe, bali ni utumwa au uhuru wa bendera tu na ambao haupaswi kuandaliwa sherehe kubwa namna hiyo.
107