Tukimulika wimbo wa Mwalimu na Wanafunzi tunapata maudhui yanayopingana na mkabala wa kiubwege Wimbo huu unabeba ujumbe wa kihalisia kuhusu bara la Afrika Malighafi za Mwafrika ni nyingi lakini Mwafrika amezidi kuteseka na kutawaliwa na Mzungu kwa miaka mingi sasa. Mwandishi analikejeli bara la Afrika kwa kulilinganisha na tajiri aliyelala na kuacha mali yake ikiibiwa na watumishi wake Wanaimba hivi:
Tajiri kashiba,
Kashiba, kashiba Ndiyo maana kalała Ashibaye hulała Huku wengine humpakuwa Ah-kuvumbua kwa nini?
Alalaye hafikiri, huota!
Ah-kuvumbua kwa nini?
Alalaye huvumbua ndotoni Ah-na kuunda kwa nini?
Alalaye huunda ruwiyani.....
(uk. 34)
Hali hii ya Waaffika kufurahia uhuru wa bendera na kusherehekea kulała kwao huku wakitegemea vya ng’ambo hubainika pia katika wimbo mwingine wanaoimba Ame na Zidi katika onyesho la nane. Nchi za Kiafrika zilitawaliwa kwa miaka mingi. Baada ya kuzinduka, Waafrika walipigana vikali na kuwafukuza Wakoloni Waafrika wakaanza kujiongoza wenyewe. Badała ya kufanya wajibu wao kazini kwa kutia bidii na kurekebisha hali ya maendeleo ya bara lao, viongozi hawa waliiga mbinu na mielekeo ya Kizungu na kuitumia. Hali hii itiendelea na bado inaendelea kuzorotesha uchumi wetu; bado Mzungu anazidi kututawala kisiri Haya ni matendo ya kihalisia na yamo katika wimbo huu. Wimbo unaanza hivi
85