Mohamed anakiuka mwelekeo huu kwa kuwapa wahusika wake wazo ia wokovu kutoka kwa Mungu
Katika sura ya tano tumejadili maana ya maisha kama ambavyo imejibainisha katika tamthilia hi i Tumeonyesha jinsi mwandishi alivyoathiriwa na waandishi wakongwe wa tapo la ubwege na hivyo kuyaona maisha ya binadamu kama usumbufu usio na maana yoyote kwake
Sawa na Beckett na Ionesco, Mohamed amebainisha kwamba maisha ni duara, ni mzunguko. Amepuuza suala la ploti na badała yake kusawiri wahusika ambao hawatendi lolote la maana ila kuzunguka kwenye pango duni lililojaa matatizo.
Aidha, tumeyajadili maswala ya kufikiri na ukweli. Kiubwege, ukweli na kufikiri ni mambo ambayo yamemshughulisha binadamu kwa muda mrefu Friedrich Nietzsche1 alisisitiza kuwa binadamu ni sharti ajizatiti katika tendo la kufikiri iii aweze kujielewa. Hata hivyo binadamu hana uwezo huo ndiposa ameshindwa kutambua ukweli kuhusu maisha yake.
Ukweli kuhusu maisha ya binadamu upo lakini umemkwepa binadamu kokotę kule anakoutafuta Wamock (1970:78) anaeleza kuwa ukweli upo kwa kila mtu na ni wajibu wetu kuutafuta. Katika Amezidi, ukweli unapatikana katika kifo. Kifo cha Zidi kinamfanya Ame kugundua ukweli juu ya uhusiano wao na EC.
Katika kushughulikia maisha. mwandishi pia ameonyesha kuwa tofauti kati ya maisha na kifo ni nyembamba mno. Tumeonyesha jinsi alivyoshughulikia suala la kifo kwa kulipatia nafasi kubwa katika Amezidi. Hivyo basi Mohamed anashangilia kifo sawa na waandishi wa tapo la ubwege.
Amezidi kwa ujumla ni tamthilia inayokatisha tamaa. Wafula (1999:69) anaeleza kuwa mwito wa kutokata tamaa haupatikani katika tamthilia ya Amezidi Inabainika kuwa, mwandishi amekasirikia ashabu wote wanaoishi barani Afrika Ingawa kimalizio cha tamthilia hii - “Wimbo wa Mtoto Asiyezaliwa” kinatuarifu kwamba
115