Uchambuzi huu umetufaa kwa kutupatia miale ya mawazo ya waandishi wa kibwege licha ya kwamba haukuzama wala kutumia mikakati ya kitaalamu
Sarara (1997)6 ameshughulikia maudhui katika tamthilia tatu za Said Ahmed Mohamed -Pungwa (1988), Kivuli Kinaishi (1990), na Amezidi (1995). Uhakiki huu umetoa mchango kwa utafiti wetu licha ya kwamba mhakiki amejikita katika maudhui tu, na kwamba kipengele cha ubwege hakijitokezi katika kazi yake
Njogu na Chimerah (1999) wametoa maelezo kuhusu Amezidi kama tamthilia ya kibwege. Wamebainisha na kufafanua kwa kifupi baadhi ya vipengee vinavyoendeleza ubwege kama vile wahusika, tamaa na matumaini. Ni kazi ambayo imenufaisha utafiti wetu ingawa wachambuzi hawakutumia nadharia yoyote
Uhakiki wowote ule una manufaa yake. Hivyo basi hatuwezi kupuuza mchango wa wenzetu kama Vuzo, Maneno, na Wafula, ambao wamejikita zaidi katika maudhui na fani. Hivi ni vipengee muhimu chambilecho Ngara (1990:5) ambaye anasema kuwa iii kuelewa kazi ya sanaa, msomaji anapaswa kufahamu yaliyomo na fani yake.
Ni matumaini yetu kuwa, kwa kutumia nadharia mahususi, sisi tutapiga hatua kubwa zaidi mbele katika kuihakiki tamthilia ya Amezidi kama kazi ya kiubwege
1.8 MSINGI WA KINADHAR1A
Nadharia ni chombo muhimu kwa mhakiki kwa vile ndiyo hutoa mwongozo bora wa utafiti Utafiti wetu utaelekezwa na kuongozwa na nadharia ya udhanaishi.
A Dictionary of Literary Terms (1977: 251) inafafanua udhanaishi ifuatavyo:
Kwa misingi ya kifalsafa, udhanaishi hujikita
katika maoni ya hali na maisha ya mwanadamu, mahali pakę na jukumu lakę katika dunia pamoja na mahusiano yake, au ukosefu wa mahusiano hayo na Mungu. (Tafsiri yetu)
11