Elimu katika ulimwengu wa mabwege hukosa misingi thabiti ya kijamii Mara nyingi huwa ni elimu ya kuigwa na ambayo haisaidii binadamu kuboresha maisha yake, bali husaidia katika kumwangamiza zaidi.
Katika tamthilia ya Amezidi, Mwalimu na Wanafunzi wake wanalala darasani na kati yao,
hakuna anayeweza kumwokoa mwenzake kutoka janga la kutojua. Ni hali ambayo inazidi
kubomoa nchi ya Amezidi kwa kukosa viongozi wenye ujuzi wa kuleta maendeleo. Hali hii
¥
hukaribiana na tunayopata katika tamthilia ya Ionesco, The Lesson Mhusika Pupil, anapatiwa elimu ambayo haimsaidii kukua wala kuimarisha maisha yake, elimu anayopata inamnyooshea mkono wa maangamizo, kifo Mwandishi anatupatia elimu isiyo na maana kwa jamii ndiposa Pupil, anauawa na Professor.
Katika onyesho la nne, tunaonyeshwa dhahiri matatizo yanayoikumba sekta ya elimu barani Afrika. Nchi ya Amezidi, inafuata mfumo wa elimu ya kigeni ambao haufungamani na mazingira yake Tunaambiwa na Mwanafunzi
Hivi ... hivi baada ya kukariri mawazo ya Archimides kwa miaka mingi, kwa nini hatujaweza kuunda nyambizi?
(uk. 30)
Ni swali ambalo viongozi wa Kiafrika wanapaswa kujibu, lakini hata wao hawana mwelekeo, ni mabwege. Mwalimu hajui jibu lakę ndiposa wanafunzi pamoja naye, wanalia na kucheka kuashiria mtafaruku wa mtazamo wa elimu hii Hapa tunapatiwa Mwalimu ambaye tunatarajia amepata mafunzo ya kutosha kuelekeza wanafunzi, lakini anashindwa kutekeleza wajibu wake Anafundisha mada ambayo haielewi na kushindwa kujibu maswali ya wanafunzi Ni mwalimu asiyefuata maadili ya ualimu Anasinzia darasani kuonyesha ubwete wake Aidha, anaingia darasani na bakora ndefu. Labda bakora ni silaha yake ya kuogofya baadhi ya wanafunzi wasimwulize maswali na kumsumbua kichwa. Mazingira ya darasani yanachukiza:
46