3.0 SURA YA TATU
3.1 UTANGULIZI
Katika sura hii tumedhamiria kuonyesha jinsi tamthilia ya Amezidi ilivyoathiriwa na mkabala wa uandishi wa kiubwege Sura hii imejikita katika vipengele mbalimbali vya kimaudhui vikiwemo dhamira ya tamthilia, suala la Mungu, suala la historia, elimu na mkengeuko. Tumevihakiki na kuvichanganua vipengele hivi na vingine zaidi iii kubainisha kiwango cha ubwege katika tamthilia hii.
3.2 DHAMIRA YA TAMTHILIA
Kimsingi, fasihi ya ubwege huwa na dhamira ya kuonyesha ubatili wa matendo ya binadamu ulimwenguni Hususan, hutumia wahusika vibonzo ambao hukosa uwezo wa kujielewa na kufikiria licha ya kutekeleza yasiyo na maana Binadamu husawiriwa kama kinyago kisicho na uwezo wa kubadilisha hali yake. Muhimu kwa binadamu ni kukaa na kusubiri kifo; kifo ambacho ndicho hatua ya mwisho ya maisha yake.
Dhamira ya Mohamed, katika Amezidi kwa maoni yetu haiafikiani kwa kiasi kikubwa na dhamira ya aina hii Mwandishi huyu yaelekea anasukumwa na dhamira ya namna ambavyo bara la Afrika limenyonywa na kuathiriwa vibaya na mataifa ya Kimagharibi yaliyoendelea Wafula (1999:75) anasema:
Tamthilia ya. Amezidi inazungumzia ukosefu wa maendeleo barani Afrika. Mwandishi anadai kwamba mataifa ya kisasa barani Afrika yamejengwa kwa uigaji kikasuku wa teknołojia za Kimagharibi, ufisadi na unafiki.
Hali hii ni ya kiuhalisia zaidi na inapingana na mtazamo wa kiubwege Madhumuni ya Mohamed, yaelekea ni kuzindua na kuhamasisha viongozi wa bara hili na raia wake kwa ujumla kuwa wazalendo kwa kulipenda bara lao na kujitolea kulifufua kimaendeleo Nchi nyingi za bara la Afrika ziko huru lakini bado zinategemea misaada kutoka ng’ambo. Mtu au nchi huru ni ile inayoweza kujitegemea na aghalabu kukimu haja zake za kimsingi Tunapoona Ame na Zidi wakiomba vitu vingi chakula
35