9058010064

9058010064



Fasihi ya ubwege hujaribu kubainisha ukweli juu ya maisha ya binadamu ulimwenguni Webb (1972:23) anasisitiza kuwa, fasihi ya kiubwege ni dhihirisho la hali ya fikra za binadamu. Binadamu anajaribu kutafuta ukweli, lakini fikra zake zinamfanya hasiupate Drama ya kiubwege hukusudia kuonyesha kushindwa kwa binadamu kujielewa yeye pamoja na hali yake ulimwenguni.

2.5.3 DHANA NA SIFA ZA DRAMA YA KIUBWEGE

Drama ya kiubwege ni aina ya drama ambayo hujitenga au hujaribu kuvuruga vipengele vya kijadi vya uandishi wa drama Tangu enzi za Aristotle, tamthilia (drama) zimebainisha utaralibu fulani wa uandishi. Drama ya kiubwege huvunja utaratibu huo, sawa na kukaidi hali ambazo hutambuliwa kama za kiuhalisia

Esslin Martin, mhakiki sifika wa tapo hili, ametoa muhtasari wa hali ya tamthilia za kiubwege5 Anaeleza kuwa ikiwa tamthilia ni lazima iwe na hadithi inayofululiza vizuri, tamthilia za kibwege huwa hazina hadithi au ploti inayoweza kuelezewa kikamilifu; kama hadithi nzuri huamuliwa kwa usawiri na umotishaji mzuri wa wahusika wake, hizi mara nyingi hukosa wahusika wa kutambulika vyema na badała yake hubainisha wahusika batili tu. Kama tamthilia ya kawaida inapaswa kuwa na maudhui pevu, hizi hukosa muwala wa maudhui Tamthilia za kibwege huwa na ndoto au ruwaza nyingi bila kumulika hali ya maisha kiuhalisia. Kawaida, tamthilia huwa na umantiki wa mazungumzo kati ya wahusika, ilhali za kibwege hubainisha utengano, upweke wa mazungumzo.

Baadhi ya waandishi wa drama ya kiubwege na ambao wameandika tamthilia zinazobainisha mtazamo wa Esslin Martin, ni Eugene Ionesco, The Killer, The Chairs, The Lesson, Rhinoceros Samwel Beckett, Waitmg for Godot, End gamę, Fernando Arrabal, Arthur Adamov, Harold FHnter na Edward Albee ambaye ameandika The Sandbox..

Kuhusu uigizaji wa drama ya kiubwege, Anderson (1972:2) anasema

Hadhira wanakumbwa na visa vingi visivyo na muwala, na matukio ya mchezo hayana maana kisaikolojia na pia katika muktadha wa matendo ya tamthilia. (Tafsiri yetu)

29



Wyszukiwarka

Podobne podstrony:
Mtindo wa tamthilia zetu umetokana na ule wa fasihi ya Kiingereza ambayo ililetwa kwetu na elimu ya
Kiudhanaishi, maisha ya binadamu husawiriwa kama fujo Hali hii hubainika kupitia shughuli mbalimbali
Mawazo haya ya Sartre na Nietzsche juu ya Mungu, yalikuwa yamedhihirika awali hasa kupitia Pascal (F
kama kazi ya kiubwege Ubwege ni tapo la kifasihi linalofuata falsafa ya udhanaishi Mwingiliano huu k
Hali hii humpatia binadamu picha halisi juu ya maisha yake yasiyo na utaratibu wowote ulimwenguni. M
Kundi la kwanza lilijikita zaidi katika matumizi ya yaliyomo katika tamthilia kudhihirisha dhana ya
kama kazi ya kiubwege Ubwege ni tapo la kifasihi linalofuata falsafa ya udhanaishi Mwingiliano huu k
skanuj0009 (405) IM..    jg a wv) xU&. -4 i- ?ya>lo-1 fioŁ-HyulA 1 iii -i- łud
skanuj0010 (67) • Wektory Współrzędne wektora AB, który przesuwa punkt A na punkt B: AB = [xB-xA,yB-
skanuj0011 (57) • Trójkąt Pole trójkąta ABC o wierzchołkach A = (xa, yA), B = (xb, yB), C = (xc,yc),

więcej podobnych podstron