Tamthilia ya Amezidi inabainisha mazingira ya kibunilizi yenye ishara mbalimbali za kiuasilia Onyesho la kwanza linaeleza:
Tendo linatokea mawazoni na uhalisini.......
Pangoni.... spotilaiti inafuata wahusika.
(Uk. 4)
Tunaambiwa kuwa Ame na Zidi wanaishi pangoni. Mazingira ya pango ni machafu na ya kinyama. Hali ya binadamu kuishi pangoni badała ya nyumbani ni dhana ya kiubwege. Binadamu husawiriwa kama kiumbe duni na anayestahili kuishi katika mazingira machafu na yanayokatisha tamaa. Katika onyesho la pili, tunaelezwa:
Zidi: Umeniamshia nini?
Ame: Kukuuliza Zidi: Nini?
Ame: Kama umepata kuikagua kwa macho nyumba hii yetu
Zidi: Humu pangoni0
Ame: Pangoni, au kasrini mwetu?
Zidi: Ah, kasri ndiyo, kwani lina nini?
(uk. 12)
Wahusika hawa wanaishi katika mazingira ya kuchukiza, pangoni, lakini wanafurahia hali hiyo. Kwao, pango ni kasri, ni makao mazuri ya kuishi. Kuishi na kufurahia uduni wa maisha ni suala la kiubwege ambalo huendeleza imani ya kidhanaishi kuwa maisha hayana maana, hayana furaha ila huzuni tupu
Hali hii katika Amezidt inakaribiana na ile inayosawiriwa katika Waitmg for Godot. Vladimir na Estragon wanatumia kichunguu kama kiti, na mchezo unafanyika barabarani Kichunguu sawa na pango ni vitu vyenye uasilia Matumizi ya vitu au vifaa vya kiasili licha ya kuweko kwa vile vya kisasa kama viti na nyumba, ni kipengele cha ubwege Barabarani ni mahali pachafu; ni mazingira yanayozua taswira ya vumbi wakati wa kiangazi na matope wakati wa mvua Beckett anapotumia barabara ya mashambani, badała ya barabara ya kisasa, ya kimji, anaendeleza hali ya kutobadilika kwa binadamu Binadamu bado anaendelea kuishi kinyama katika maisha yenye usumbufu na yanayokatisha tamaa.
69