Hili ni pango linalokatisha tamaa. Wakazi wake ni maskini sana kiasi cha kukosa malazi mema. Wanalalia majani ambayo ndiyo godoro lao. Mwandishi anatuambia kwamba licha ya uduni huu wa kimaisha , wakazi hawa wanafurahia hali na mazingira yao na ndiposa tunamkuta Zidi amelala usingizi wa pono , usingizi anaoupenda bila shaka
Mohamed ana wazo kuwa, tangu Mwafrika aanze kuishi ulimwenguni, hajabadilisha nyumba vake Bado anaendelea kuishi na kusherehekea pango lakę Licha ya kuwa maisha yao ni sawa na ya mnyama , Ame na Zidi , hawafanyi Jolote kujikwamua kimaisha Wanabaki wakizembea kazi na kutegemea misaada ya kigeni Kejeli ni kwamba, hata misaada hiyo ni duni na haina manufaa ila kuendeleza uduni wao katika pango.
Pango pia linageuka na kuwa ofisi, na hata darasa. Mabadiliko haya ni ya kimawazo tu, si ya kihalisia, kwa vile pango ni lile lile lenye mazingira ya kuchukiza.
Katika onyesho la nne tunaambiwa:
Tendo limo fikirani . pangoni ...Tendo la shuleni.Zidi ni mwalimu , kaketi mbele ya meza ambayo haionekani.Pana ubao na chaki ambavyo havionekani Ame (mwanafunzi) ameketi kwenye deski lisiloonekana pia.Kuna wanafunzi wapatao sabini.Pia hawaonekani ila Ame tu! Mwalimu. Zidi anasinzia huku darasa limejaa zogo la wanafunzi... kitambo . . kisha kengele inasikika kulia .. Mwalimu Zidi anashtuka kutoka usingizini...)
(uk.29)
77