Hili ni pango linalokaribiana sana na pango tulilopatiwa awali Ingawa mwandishi amelibadilisha kuwa darasa, bado hali ya uduni na utupu inaendelea kubainika. Mandhari ya shule yanafaa kuwa na vifaa muhimu vya kimasomo, mwalimu mwenye ujuzi na uwezo wa kumiliki darasa, pamoja na wanafunzi watiifu. Hali inayosawiriwa ni kinyume kabisa na matarajio hayo. Hamna ubao, deski na chaki ila zile za kimawazo tu! Mwalimu mwenyewe hatambui wajibu wake, amelala Kulała kwake ni sawa na kule kwa Zidi katika onyesho la pili. Tabia ya kulała haijabadilika. Zidi katika onyesho la pili anaamshwa na Ame, na Mwalimu anaamshwa na mlio wa kengele Kwa upande wao, wanafunzi ni zogo si watiifu na hawatambui kuwa warno darasani. Tena ni wanafunzi wengi sana, sabini, idadi ambayo ni kubwa na ngumu kwa mwalimu mmoja wa somo la fizikia. Haya ni mazingira yasiyopendeza na yanayosheheni sifa za kiubwege.
Labda mwandishi amepuuza tendo la kuyafanya mandhari haya yatangamane na hali na muktadha wa kidarasa iii kukejeli maendeleo ambayo Waafrika wanajivunia. Nchi nyingi za bara hili zimesahau wajibu wao wa kusanifu maendeleo, na hivyo kubaki zikitegemea misaada kutoka mashirika ya kigeni Katika onyesho la nane, Ame na Zidi, wanasemezana:
Ame: Tumelala au tu macho?
Zidi: Sijui.
Ame: Ndiyo ujue tu !
Zidi: Madawa tununue? kwa nini hatufanyi yetu? Ame: Si mpaka tuvumbue kwinini!
Zidi: Kwa nini hatuvumbui ?
Ame: Tununue tu!
Zidi: Kwa nini?
Ame: Ndiyo raha, ndiyo kuendelea.
Utafiti wa nini? Uvumbuzi wa nini?
Si tununue tu , tuna fedha bwana !
(uk.66)
78